-->

Change Language

Watatu Kufyekwa Tena Yanga SC

Post a Comment

 

 

Tovuti maarufu ya michezo nchini Tanzania imechapicha taarifa inayoeleza kuhusi klabu ya Yanga Sc kuachana na wachezaji wake watatu hivi karibuni.

Mwanaspoti Wameandika,

"Mwanaspoti lilishawatarifu mapema kwamba, Miguel Gamondi ametua na faili zito la kufyeka baadhi ya mastaa waliosalia kikosini wakiwamo wakigeni na wale wazawa, lakini mtu wa kwanza ambaye anaweza kwenda na maji ni beki mahiri, Djuma Shabani 🇨🇩"


"Beki huyo anatajwa kuwa ni mchezaji aliye kwenye rada ya kupitiwa na panga, kwani jina lake (Kufyekwa) lilikuwapo tangu enzi za Kocha Nasreddine Nabi."


"Nabi aliyeipa Yanga mataji saba yakiwamo mawili ya Ligi Kuu, mengine mawili ya ASFC na Ngao ya Jamii mara mbili pamoja na Kombe la Mapinduzi, inaelezwa alishatoa mapendekezo mapema juu ya wachezaji wa kuachwa kwa msimu ujao na majembe mapya ya kuingia kabla ya Gamondi kuajiriwa na klabu ya Yanga,"


"Hata hivyo mapema Gamondi aliuambia uongozi uzuie wachezaji kadhaa wasiondoke kikosini baada ya kupitia video ya mechi tano za mwisho za msimu uliopita zikiwamo mbili za fainali ya CAF, lakini baada ya kuchungulia tena video hizo amebaini kuna watu wa kutemwa tena."


"Na kati ya wachezaji waliongia kwenye 18 za panga jipya, litakalotegemea na kocha Gamondi mara atakapokutana na mabosi wa klabu hiyo kuweka mambo sawa ni pamoja na Djuma Shabani"


"Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Yanga kinasema kinachomponza Djuma ni kudaiwa ni mmoja kati ya wachezaji waliokuwa wakiendesha migomo ya chini chini klabu na kumchefua Nabi, huku mwingine akitajwa ni kiungo Yannick Bangala anayeweza pia kufyekwa na panga hilo jipya."


"Kuna asilimia kubwa kwa Djuma kwenda na maji, lakini tunasubiri kwamba kocha aje tumsikilize maamuzi yake, lakini jina jingine lililo kwenye hatari hiyo ni Bangala (Yannick), pia kuna wazawa kadhaa wanaoweza kupewa 'thank you' na kupelekwa kwa mikopo klabu nyingine," kilisema chanzo 


"Kabla ya panga hilo lijalo, Yanga ilishawapa 'thank you', Dickson Ambundo, Abdallah Shaibu 'Ninja', Erick Johora, Bernard Morrison na Tuisila Kisinda aliyerejeshwa klabu ya RS Berkane baada ya kuitumikia Yanga kwa mwaka 1."

 Chanzo: tovuti ya Mwanaspoti. 

Related Posts

Post a Comment

Join Us Free, in Telegram.

Subscribe Our Newsletter