-->

Change Language

Alicho Fanyiwa Manula Wa Simba SC Akiwa Anatoka Hospital

Post a Comment


 KUTOKA KWA @MANULA


Baada ya kufanya vipimo hospital ya Taifa MUHIMBILI-MLOGANZILA nilianza safari ya kurudi nyumbani kwetu KILOMBERO 

Nilifika morogoro mjini mishale ya saa kumi na moja na dakika kumi na nane hivi. Nilipata mapumziko kidogo kisha tukaendelea na safari ya kwenda KILOMBERO.

Tukapita mindu,melela na vijiji vingine vingi kisha tukafika DOMA. Nikamwambia mwalimu{dereva} simamisha gari hapo kwenye hizo mali shamba ili tununue nyanya, hoho, vitunguu nak.

Akasimama kisha akashuka kwa ajiri ya kununua vile nilivyohitaji.akaagiza na kuvipakia kwenye gari na baada ya kumaliza akamuambia mmoja wa wauzaji kuwa nenda kule mbele ukapewe pesa zenu.


Alikuja dada mmoja na nikashusha kioo cha gari na kumuuliza ni kiasi gani, baada ya muuliza akanijibu lakini akionyesha na kushangazwa kisha akatoa sauti kubwa akiambia wenzako kuwa “jamani manula huyu) huku akinipa chenji yangu.

Dakika moja nyingi ndugu zangu wajasiliamali na wengi wao ni akina dada na akina mama walikuja kwa wingi huku wakionyesha furaha zao kwa kuniona. Walinipa pole za kutosha na kusema tunakuombea dua upone haraka.

Ghafla….
Wakaanza kuniletea nyanya, vitunguu, maharagwe, matango, nyanya chungu, 
Bila kujali wakaanza kunipa na fedha yani mwenye buku,mwenye buku mbili 
Haikutosha wakaanza kuimba kwa furaha na shangwe.

Hakika mapenzi yako yalinifanya nishuke nikiwa na magongo yangu mkononi na kuwashukuru kwa upendo wao, kisha tukapata picha ya kumbukumbu.

Nikaendelea na safari ya kwenda nyumbani na nilipofika nyumbani nikakuta vitu walivyonipa bure ni vingi kuliko nilivyo nunua na pesa waliyonipa ni nyingi kuliko niliyotoa kunuanulia.

Ahsanteni sana mama/dada zangu wa DOMA kwa upendo wenu kwa mimi kijana wenu. MWENYEZI AZIBARIKI KAZI ZA MIKONO YENUW

Related Posts

Post a Comment

Join Us Free, in Telegram.

Subscribe Our Newsletter