Ratiba ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania 2025/26: Kariakoo Dabi ya Kwanza Desemba 13
Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara msimu wa 2025/26 inatarajia kuanza rasmi Septemba 17, 2025, ikishirikisha timu zote vigogo na wapinzani wa jadi wa soka la Bongo.
Mechi za Ufunguzi
KMC FC vs Dodoma Jiji FC – Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam
Coastal Union vs Tanzania Prisons – Uwanja wa Mkwakwani, Tanga
Mashabiki wa soka wanatarajia mtanange wa kusisimua mara tu msimu utakapoanza, huku kila timu ikihitaji kuanza na pointi tatu muhimu.
Kariakoo Dabi: Simba SC vs Yanga SC
Vigogo wa soka la Tanzania, Simba SC na Yanga SC, watakutana kwa mara ya kwanza katika msimu mpya wa Ligi Kuu ya NBC 2025/26 mnamo Desemba 13, 2025, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huu, Yanga SC watakuwa wenyeji.
Dabi ya marudiano itapigwa tena Aprili 4, 2026, ambapo safari hii Simba SC watakuwa wenyeji. Kariakoo Dabi inabaki kuwa mchezo unaovutia mamilioni ya mashabiki ndani na nje ya Tanzania, na msimu huu unatarajiwa kutoa burudani ya kipekee zaidi.
Mashabiki wote wanatazamia msimu wa Ligi Kuu NBC Tanzania 2025/26 wenye ushindani mkubwa, michezo mikali na burudani ya kiwango cha juu. Je, ni nani ataibuka kinara kati ya Simba SC, Yanga SC, Azam FC na timu zingine zinazokuja juu?
Www.SokaLetu.Com
0 Comments