-->

Change Language

Mayele Kuondoka Yanga | HATMA YA YANGA NA MAYELE

Post a Comment

 

Mayele Yanga

Mayele Kuondoka Yanga | HATMA YA YANGA NA MAYELE


Mayele ana magoli mangapi, Mayele salary, Mayele photo, Mayele Kuondoka Yanga, Mayele to Kaizer Chiefs, Mayele Transfer Update


LEO ndio ile Siku ya kikao kati ya Uongozi wa Yanga na Mshambuliaji Fiston Mayele kwaajili ya kujadiliana kama Mayele ataondoka au atabakia ndani ya timu hiyo.

 Kutokana na mahojiano aliyofanyiwa mayele na moja ya chombo cha habari cha nchini Tanzania, Mayele alifunguka na kusema kuwa, Hatima ya yeye kuondoka au kubaki itajulikana jumatatu baada ya uongozi kukaa na Yeye kujadiliana kuhusu malipo.

Ikumbukwe kuwa, kinacholeta ugumu mpaka sasa kwa Yanga SC kumalizana na mayele ni kuhusu mshahara. Yanga imetoa ofa ya zaidi ya milioni 35 huku Fiston Kalala Mayele akiomba kuongezewa angalau zifike milioni 40.

Mayele ambaye ni mfungaji bora wa NBPC PREMIER LEAGUE na nyota mwenye tuzo nyingi katika soka anasema kuwa mpaka sasa ameshapokea Ofa nyingi kutoka kwenye klabu mbalimbali ikiwemo timu iliyotoa ofa ya Rand milioni 22 (Sawa na Sh 2,806,936,000) kwaajili ya Fiston Mayele kujiunga na Sepahan SC ya nchini Iran.


Mayele amekuwa katika kiwango bora kwa misimu miwili aliyoitumikia Yanga ambapo msimu wa 2022/23, ametangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Bara.


Mtandao mmoja kutoka Afrika Kusini, umeripoti jumla ya klabu tatu zimeonesha nia ya kuhitaji saini ya mshambuliaji huyo ikiwemo Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.


Klabu hizo zinapata ugumu kutokana na mkataba wa mwaka mmoja alionao Yanga, ambao ameusaini katikati ya msimu uliomalizika.


Licha ya mkataba huo, lakini meneja wa Mayele pamoja na uongozi wa Yanga umesema upo tayari kusikiliza ofa kutoka kwa klabu hizo.


Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said, alibainisha kwamba: “Bado hatujapokea taarifa yoyote kutoka Afrika Kusini, na hakuna klabu hata moja iliyowasiliana nasi.”


Wakala wa Mayele, hivi karibuni alizungumzia hilo akisema klabu pekee ya Afrika Kusini iliyoonesha nia ya kumtaka mshambuliaji huyo ni Mamelodi Sundowns.


“Kwa sasa, tuna ofa mbili thabiti mezani kutoka Saudi Arabia na Afrika Kusini. Hatujazizuia klabu nyingine kuanza mazungumzo na ofa inayotuvutia zaidi ni Rand 22.2 Mil (zaidi ya Sh 2.8Bil za Kitanzania) na nyingine ni Rand 13Mil (zaidi ya Sh 1.6Bil za Kitanzania) ambazo tumezipata kutoka katika klabu hizo zilizoonyesha nia,” alisema. Source - ©Global Publishers


Hivyo hatma ya Mayele na Yanga kujulikana leo baada ya kikao na soka letu tuko hapa kuwajuza.


Related Posts

Post a Comment

Join Us Free, in Telegram.

Subscribe Our Newsletter