-->

Change Language

ROBERTINHO - Wapinzani Hasa Yanga na Azam FC Kukiona Cha Moto

Post a Comment

 

ROBERTINHO -" TIMU IMEKAMILIKA

YANGA, AZAM KUKIONA CHA MOTO"



Kocha Wa Simba SC iliyopo Tanzania, Robertinho alisema amekoshwa sana na namna mabosi wa Simba walivyotekeleza mapendekezo yako kwenye usajili kwani umeifanya timu hiyo ienee kila idara kwa sasa na kumpa jeuri ya kuamini atasumbua sana kwenye msimu ujao mbele ya wapinzani wao hasa Yanga SC na Azam FC.


Kocha Huyo alizungumza  mara baada ya kutua Uwanja wa Ndege, alisema kwa kujiamini kuwa kwa usajili ambao umefanywa, ni wazi heshima ya klabu hiyo inarudi tena baada ya kumaliza misimu miwili mfululizo bila kutwaa taji lolote mbele ya Yanga.

Mpaka sasa Simba imeshawatangaza mawinga wawili wapya, Leandre Onana kutoka Rayon Sports ya Rwanda na Aubin Krabo aliyekuwa Asec Mimosas ya Ivory Coast najana imemtambulisha  beki wa kati, Che Fondoh Malone kutoka CotonSport ya Cameroon.

Mbali na hao pia Simba inahusishwa kumalizana na mshambuliaji Fabrice Ngoma aliyekuwa Al Hilal ya Sudan sambamba na kipa Mbrazili, Caique Luiz Santos anayetua kati ya leo na kesho kabla ya Jumanne timu kusepa kwenda kambini ya maandalizi ya msimu huko Uturuki.


Source: Mwanaspoti



Related Posts

There is no other posts in this category.

Post a Comment

Join Us Free, in Telegram.

Subscribe Our Newsletter