Simba Yamnasa Nathaniel Chilambo Kutoka Azam FC, Asaini Mkataba wa Miaka Mitatu

 


Tetesi/Breaking News ya Usajili: Simba SC Yamnasa Nathaniel Chilambo Kutoka Azam FC kwa Mkataba wa Miaka Mitatu


Klabu ya Simba Sports Club imekamilisha usajili wa beki wa kulia wa Azam FC, Nathaniel Chilambo, kwa uhamisho wa bure (free transfer), hatua inayotajwa kuimarisha zaidi safu ya ulinzi ya wekundu wa Msimbazi kuelekea msimu mpya wa mashindano.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, Nathaniel Chilambo mwenye umri wa miaka 26 tayari amesaini mkataba wa miaka mitatu kujiunga na Simba SC, huku makubaliano yote yakielezwa kukamilika rasmi.

Usajili wa Chilambo unatajwa kuwa sehemu ya mkakati wa Simba kuimarisha kikosi chake, ambapo atakwenda kuongeza ushindani katika nafasi ya beki wa kulia sambamba na wachezaji waliopo kama Shomari Kapombe na Israel Duchu.

Orodha ya usajili wa Simba unaoendelea kuvuma:

  • Nathaniel Chilambo
  • Kelvin Nashon
  • Chombedo
  • ⏭️ Sopu

Mashabiki wa Simba sasa wana matumaini makubwa kuona usajili huu ukiongeza ushindani ndani ya kikosi na kusaidia timu kufanya vizuri katika Tanzania Premier League pamoja na michuano ya kimataifa.

Post a Comment

0 Comments