Clatous Chama Asaini Mkataba Mpya Simba
Kiungo mshambuliaji wa Simba Sports Club, Clatous Chama, ameendelea kuonyesha ubora wake ndani ya kikosi cha wekundu wa Msimbazi baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka miwili na klabu hiyo.
Katika siku ya kusaini mkataba wake mpya, Chama aliandika historia nyingine kwa kutoa assists mbili safi, akiiwezesha Simba kupata ushindi wa mabao 3 katika mchezo wa leo na kuthibitisha kuwa bado ni mchezaji muhimu ndani ya kikosi hicho.
Takwimu zinaonyesha kuwa hadi sasa Chama mwenye umri wa miaka 34 tayari amehusika moja kwa moja kwenye mabao 14, akiwa amefunga mabao 8 na kutoa assists 6 msimu huu — rekodi inayodhihirisha kiwango chake bora licha ya umri wake.
Mashabiki wa Simba wamepokea kwa furaha taarifa ya kuendelea kwa Chama, wakiamini uzoefu wake utaendelea kuwa silaha muhimu kwa timu hiyo katika mbio za Tanzania Premier League na michuano ya kimataifa.


0 Comments