Chino Wanaman Kuanika Burudani Simba Day 2025
Mashabiki wa Simba SC watarajie kupata burudani ya kipekee katika Simba Day 2025 baada ya kuthibitishwa kuwa msanii wa Bongo Flavor, Chino Wanaman, atapanda jukwaani kutoa shoo ya aina yake.
Chino Wanaman, ambaye kwa sasa anaendelea kufanya vizuri kwenye muziki wa Bongo Flavor, amejipatia mashabiki wengi kutokana na sauti yake ya kipekee na tungo zenye ujumbe mzito. Uwepo wake kwenye Simba Day unatarajiwa kuongeza hamasa na kufanya tukio hilo kuwa la kukumbukwa kwa wapenzi wa soka na muziki nchini.
Simba Day imekuwa ikihusisha burudani kubwa za muziki sambamba na utambulisho wa kikosi kipya cha msimu. Mwaka huu, klabu ya Simba SC imepanga kufanya tukio hilo kwa kiwango cha juu zaidi, na burudani ya Chino Wanaman ni sehemu ya kufanikisha sherehe hiyo.
Mashabiki wa Msimbazi na wadau wa burudani kwa ujumla wanatarajia kushuhudia maonyesho ya burudani, muziki, pamoja na shamrashamra zitakazopamba siku hiyo muhimu katika kalenda ya Simba SC.
Tazama HAPA wasanii wengine watakao kuwepo kwenye SIMBA DAY
SOMA ZAIDI...
0 Comments