Feisal “Fei Toto” Salum Kukamilisha Ujio Simba SC, Allan Okello Apoteza Nafasi
Simba SC wamekuwa wakimfuatilia kiungo mshambuliaji Allan Okello kwa muda mrefu, lakini kwa sasa hakuna dalili za dili lolote kukamilika. Sababu kubwa ni kwamba kikosi cha Wekundu wa Msimbazi tayari kimejaa viungo wanaocheza nafasi ya namba 10, hivyo ujio wa Okello hauna ulazima.
Badala yake, Simba wameweka mkazo kwa kumsajili Feisal “Fei Toto” Salum kutoka Azam FC. Kwa mujibu wa taarifa, Fei Toto tayari amekubaliana kujiunga na Simba, na mpango wa uhamisho wake uko wazi:
- Atasaini mkataba wa awali Januari 1, 2026
- Atakamilisha rasmi uhamisho wake mara tu mkataba wake na Azam FC utakapomalizika
Kocha wa Simba, Fadlu Davids, amekuwa akisisitiza haja ya kuwa na mchezaji mwenye tofauti (X factor) kwenye kikosi chake, na inaonekana Fei Toto ndiye anayetarajiwa kutoa ladha hiyo ya kipekee msimu ujao.
Kwa sasa, mashabiki wa Simba wanasubiri kwa hamu kuona namna Fei Toto atakavyoongeza nguvu na ubunifu katika safu ya kiungo, huku jina la Allan Okello likiendelea kufutika kwenye mipango ya klabu hiyo.
0 Comments