Yakubu Suleiman Ally na Wilson Nangu Wajiunga Rasmi na Simba SC
Afisa Habari wa JKT Tanzania, Massau Bwire, ametangaza kuwa usajili wa wachezaji wawili muhimu wa timu hiyo, Yakubu Suleiman Ally na Wilson Nangu, kwenda Simba SC umekamilika rasmi leo jioni, 28 Agosti 2025.
Katika taarifa yake, Bwire ameeleza kuwa makubaliano hayo yamefanyika kibiashara bila kubadilishana mchezaji yeyote kutoka Simba SC.
> “Hatimaye jioni hii tumekamilishana na Simba SC, sasa ni rasmi Yakubu Suleiman Ally na Wilson Nangu wanaelekea Msimbazi. Hatubadilishani mchezaji yeyote kutoka Simba, tumekubaliana kibiashara,” alisema Massau Bwire kupitia taarifa yake.
Usajili huu unaonekana kuongeza nguvu kubwa kwa kikosi cha Simba SC kinachoendelea kujiandaa kwa msimu mpya wa mashindano ya ndani na ya kimataifa.
0 Comments