Simba SC Yamleta Gomezi kwa Mkopo wa Mwaka Mmoja

 



🚨 Simba SC Yamleta Gomezi kwa Mkopo wa Mwaka Mmoja

Mshambuliaji chipukizi wa Kitanzania, Seleman Mwalimu maarufu kama ‘Gomezi’, amejiunga rasmi na klabu ya Simba SC kwa mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja akitokea Wydad Casablanca ya Morocco.

Gomezi (20) ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa, anayejulikana kwa uwezo wake wa kutumia vyema nafasi anazopata, kufunga mabao kwa miguu yote miwili pamoja na kichwa.

📌 Safari ya Soka ya Gomezi

- Kabla ya kutua Wydad katika dirisha dogo la usajili msimu uliopita, Gomezi alikuwa akikipiga Fountain Gate FC ambapo alifunga mabao 6 kwenye Ligi Kuu ya NBC.
- Amecheza pia KVZ ya Zanzibar na baadaye Singida Black Stars, hatua iliyompa uzoefu mkubwa katika Ligi Kuu Tanzania Bara.
- Aidha, ana uzoefu wa kimataifa akiwa sehemu ya kikosi cha Wydad kilichoshiriki Kombe la Dunia la Vilabu (Club World Cup) nchini Marekani, Juni 2025.

> Kinachomvutia Simba SC

Simba SC imesisitiza kuwa moja ya sababu kubwa za kumsajili Gomezi ni uzoefu wake wa ndani ya Ligi Kuu ya Tanzania pamoja na uwezo wa kucheza michezo ya kimataifa bila hofu.

📍 Yupo Dar tayari kuanza

Kwa sasa, Gomezi tayari amewasili Dar es Salaam akisubiri kurejea kwa kikosi kutoka kambi ya maandalizi nchini Misri, ili aanze maandalizi ya msimu mpya wa mashindano wa 2025/26.

Post a Comment

0 Comments