-->

Change Language

USAJILI MPYA WA SIMBA SC, ALASSANE KANTÉ!

Post a Comment

 


🔴⚪ Karibu Simba, Alassane Kanté!

Klabu ya Simba SC imemtambulisha kiungo mkabaji Alassane Maodo Kanté, raia wa Senegal, aliyejiunga rasmi na kikosi cha Simba kutoka CA Bizertin ya Tunisia kwa mkataba wa miaka miwili, ukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.

Kanté (25) ni kiungo mwenye uwezo mkubwa wa kukaba na kushambulia, akijulikana kwa pasi sahihi zinazofika kwa walengwa bila kujali umbali. Msimu uliopita akiwa CA Bizertin, alifunga mabao manne na kusaidia kupatikana kwa mengine manane (assist), akionekana kuwa mhimili mkubwa wa kikosi hicho.

Uongozi wa klabu na benchi la ufundi lina matumaini makubwa naye katika kutimiza malengo ya ndani na ya kimataifa.

Kanté anakuwa ni mchezaji wa pili kusajiliwa rasmi kuelekea msimu mpya, baada ya Simba kukamilisha usajili wa beki wa kati, Rushine De Reuck hapo jana... SOMA ZAIDI.. 


Related Posts

There is no other posts in this category.

Post a Comment

Join Us Free, in Telegram.

Subscribe Our Newsletter