-->

Change Language

Namungo Yathibitisha Kumtaka Ally Salim, Simba Yakaribia Kumtema Rasmi

Post a Comment


Namungo Yathibitisha Kumtaka Ally Salim, Simba Yakaribia Kumtema Rasmi

Hatma ya kipa wa Simba SC, Ally Salim, inaonekana kufikia ukingoni ndani ya kikosi cha Msimbazi huku klabu ya Namungo FC ikithibitisha kuwa katika mazungumzo ya kumsajili mlinda mlango huyo mwenye kipaji kikubwa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka chanzo cha kuaminika ndani ya Namungo FC, mazungumzo kati ya uongozi wa timu hiyo na Simba yanaendelea vizuri, japokuwa Salim bado ana mkataba unaomalizika mwaka 2027.

“Mkataba wa Salim na Simba unamalizika mwaka 2027. Kwa sasa kinachoendelea ni mazungumzo kati ya Namungo na waajiri wake. Licha ya kuwa bado ana mkataba, hayupo kwenye mipango ya timu hiyo kwa msimu ujao, hivyo chochote kinaweza kutokea. Anaweza kutua Namungo na kuwa sehemu ya kikosi chetu,” alisema mtoa taarifa kutoka Namungo.

Namungo wameonyesha dhamira ya kweli katika kumpata kipa huyo, wakiamini kuwa uzoefu wake utaongeza thamani ndani ya kikosi chao.

“Tunamhitaji na tunatambua uwezo wake. Tunaamini anaweza kutusaidia kutokana na uzoefu wake, japo amekuwa hapati nafasi ya kucheza mara kwa mara. Tunaamini kwamba akipewa nafasi, ataonyesha uwezo mkubwa na kufanya mambo mazuri.” - Kiliongeza chanzo hicho

Wakati hayo yakijiri, ndani ya klabu ya Simba tayari kuna taarifa kwamba Salim ni miongoni mwa wachezaji watakaotemwa katika dirisha la usajili la kuelekea msimu ujao. Imeelezwa kuwa Simba imeanza mipango ya kuboresha safu ya ulinzi langoni kwa kumsajili kipa wa JKT Tanzania, Yakubu Suleiman, ambaye anatajwa kuwa chaguo la moja kwa moja kuchukua nafasi ya Salim.

Kwa sasa mashabiki wa soka wanasubiri kuona kama Namungo itaweza kufanikisha dili hilo na kumpa Salim nafasi ya kurejea kwenye kiwango chake akiwa kama kipa namba moja.

Source: Mwanaspoti

Related Posts

Post a Comment

Join Us Free, in Telegram.

Subscribe Our Newsletter