LAMECK LAWI ATAMBULISHWA RASMI AZAM FC
Klabu ya Azam FC imefanikiwa kumsajili rasmi beki mahiri, Lameck Lawi, ambaye amejiunga na kikosi hicho akitokea Coastal Union. Mchezaji huyo amesaini mkataba wa miaka miwili na atakuwa sehemu ya kikosi kinachojiandaa kwa msimu mpya wa mashindano.
Usajili wa Lawi unatajwa kuwa ni sehemu ya mkakati wa klabu hiyo katika kuimarisha safu ya ulinzi na kuongeza ushindani ndani ya timu kuelekea kampeni zijazo.
Azam FC inaendelea kuonyesha dhamira yake ya kuwania mafanikio makubwa kwa kuleta nyota wenye uwezo na uzoefu wa kusaidia timu kufikia malengo yake.
Karibu Chamazi, Lameck Lawi!
Post a Comment
Post a Comment