-->

Change Language

Azam FC Yamnasa Lameck Lawi Kutoka Coastal Union kwa Mkataba wa Miaka Miwili

Post a Comment

 

Azam FC Yamnasa Lameck Lawi Kutoka Coastal Union kwa Mkataba wa Miaka Miwili

Azam FC imefanikiwa kumpata beki mahiri wa Coastal Union, Lameck Lawi, na kumaliza minyukano ya vigogo wengine waliokuwa wakimwania. Lawi sasa atajiunga rasmi na kikosi cha Wanalambalamba kwa msimu wa 2025-2026.

Kiongozi mmoja wa Azam FC amethibitisha kwamba Lawi tayari ametia saini mkataba wa miaka miwili, hatua inayothibitisha nia ya timu hiyo kuimarisha safu yake ya ulinzi kwa msimu ujao.

Hapo awali, Simba SC ilijaribu kumsajili Lawi kwa mkataba wa miaka mitatu, lakini mazungumzo kati yao na Coastal Union hayakufanikiwa. Mvutano huo ulifikia hatua ya kuhusisha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Azam, usajili wa Lawi una lengo la kuongeza ushindani katika safu ya ulinzi, ambapo atakutana na mabeki wa kimataifa kama Yeison Fuentes kutoka Colombia na Yoro Diaby. Lawi anatarajiwa kuwa chachu muhimu kama beki mzawa katika kikosi hicho.

Aidha, Azam inatarajiwa kufanya tathmini ya Abdallah Kheri, aliyekuwa akicheza Pamba kwa mkopo, ili kuamua kama anastahili kuongezwa nguvu katika nafasi hiyo. 


Related Posts

Post a Comment

Join Us Free, in Telegram.

Subscribe Our Newsletter