MO DEWJI ATOA TAARIFA NZITO KUHUSU SIMBA SC

 

MO DEWJI AJIHUZULU UENYEKITI WA BODI YA SIMBA


Taarifa iliyotolewa na Mo Dewji inasema

Ndugu wanachama, wapenzi na wadau wa Simba Sports Club,

Kwa muda mrefu nimekuwa nikihudumu kama Rais wa Simba SC na Mwenyekiti wa Bodi. Hata hivyo, kutokana na majukumu yangu mengine na ukweli kwamba mara nyingi nipo mbali, nimeona ni muhimu klabu yetu ipate kiongozi wa bodi ambaye yupo karibu, mwenye muda wa kutosha na anaweza kushiriki kwa ukaribu zaidi katika shughuli za kila siku.

Kwa msingi huo, ninatangaza rasmi kwamba nitaendelea kubaki kama Mwekezaji na Rais wa Simba SC, lakini nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi sasa inakabidhiwa kwa kiongozi mpya.

Ningependa pia kutumia nafasi hii kuwashukuru kwa dhati wajumbe wote wa bodi waliotumaliza kwa uongozi wao, muda na mchango wao mkubwa katika maendeleo ya Simba SC. Kila mmoja wenu ameacha alama ya kipekee katika safari ya klabu yetu.

Kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Kampuni (MEMARTS) ya Simba Sports Club Company Limited, Ibara ya 41, Rais anatokana na MO Simba Company Ltd na anayo mamlaka ya kufanya uteuzi wa viongozi wa Bodi. Kwa mamlaka hayo, nimeamua kumteua Ndugu Crescentius Magori kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Klabu ya Simba SC.

Aidha, kwa mujibu wa ibara hiyo hiyo, nimewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi upande wa Mwekezaji:

  • Barbara Gonzalez – Mjumbe wa Bodi
  • Hussein Kiita – Mjumbe wa Bodi
  • Azim Dewji – Mjumbe wa Bodi
  • Rashid Shangazi – Mjumbe wa Bodi
  • Swedi Mkwabi – Mjumbe wa Bodi
  • Zuly Chandoo – Mjumbe wa Bodi
  • George Ruhangoo – Mjumbe wa Bodi

Nina imani kuwa kwa pamoja, timu hii mpya ya uongozi italeta msukumo mpya na kuendeleza ndoto ya Simba SC ya kuwa klabu bora barani Afrika.

Asanteni kwa uungwaji mkono wenu endelevu.

Mohammed Dewji (Mo)
Mwekezaji & Rais – Simba Sports Club. 

Post a Comment

0 Comments