RASMI: Rushine De Reuck ni Mnyama
Mlinzi wa kati, Rushine De Reuck amejiunga na kikosi cha Simba SC kutoka Mamelodi Sundowns kwa mkataba wa mwaka mmoja huku kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.
Tue, Jul 29
De Reuck (29) raia wa Afrika Kusini ni mlinzi mwenye uzoefu mkubwa wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na hiyo ni moja ya vitu vilivyo washawishi Simba SC kuisaka saini yake.
Msimu uliopita De Reuck alikuwa anachezea timu ya Maccabi Petah Tikva ya Israel na alikuwa moja ya wachezaji muhimu ndani ya kikosi hicho.
Huu ni usajili wa Simba wa kwanza kuelekea msimu mpya wa mashindano 2025/2026 na tayari amewasili nchini kuanza maandalizi (Pre Season). SOMA ZAIDI...
Post a Comment
Post a Comment