TETESI: Yakubu Suleiman Aingia Kwenye Radar za Simba SC – Rekodi Zake Zavutia Msimbazi
Kipa wa JKT Tanzania, Yakubu Suleiman, anatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji wanaowaniwa na klabu ya Simba SC kuelekea msimu mpya wa 2025/26.
Taarifa kutoka chanzo cha kuaminika ndani ya uongozi wa klabu hiyo zimeeleza kuwa tayari Simba imeonyesha nia ya wazi ya kutaka kumsajili mlinda mlango huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri akiwa na JKT kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, rekodi nzuri za Yakubu Suleiman msimu uliopita ndizo zilizowavutia mabosi wa Simba, ambao kwa sasa wako katika harakati za kufanya mabadiliko ya kikosi chao ili kuimarisha safu ya ulinzi, hususan langoni.
Yakubu amekuwa na kiwango bora msimu huu, akiokoa penalti muhimu na kuonyesha utulivu mkubwa langoni hata dhidi ya timu kubwa. Umahiri wake umeonekana si tu kwenye mechi za kawaida, bali pia katika mechi za presha kubwa, jambo ambalo limefanya jina lake kuwa kwenye orodha ya wachezaji wanaopewa kipaumbele katika dirisha lijalo la usajili.
Endapo dili hilo litakamilika, itakuwa ni hatua muhimu kwa Yakubu Suleiman kujiunga na moja ya klabu kubwa Afrika Mashariki, huku akitarajiwa kuongeza ushindani mkubwa katika nafasi ya kipa ndani ya kikosi cha Simba SC.
Post a Comment
Post a Comment